Walarasi (kutoka Kiing.: walrus, pia huitwa nguva aktiki au sili-pembe; Kisayansi: Odobenus rosmarus) ni mnyama mkubwa wa Bahari ya Aktiki anayefanana na nguva wa kawaida mwenye meno mawili marefu, yanayoitwa pembe pia, kama tembo.
Neno la "walarasi" linatoka neno la Kiingereza "walrus" litokalo labda maneno ya Kiholanzi "walvis" (nyangumi) na "ros" (farasi) lakini inawezekana zaidi kwamba walrus linatoka neno la Kinorwei cha Kale "hrossvalr". Jina la "nguva aktiki" linatoka neno la nguva kwa sababu mara nyingi mnyama huyu amechanganyikwa na nguva halisi. Huitwa "sili-pembe" kwa sababu mnyama huyu ana mnasaba na sili (wako pamoja katika kundi la kitaksonomia la Pinnipedia).
Vifuko vya hewa chini ya koo shingoni mwa walarasi, shingo lililo fupi na nene, vifuko hivyo vina uwezo wa kuvimba na hewa ili kumpa uwezo wa kuelea wima na kichwa chake juu ya maji. Pia vinatumiwa kama vyumba vya mvumo vinavyotoa sauti kama kengele chini ya maji. Kinyume ya vikono vya nyuma, haya ni marefu kama yaliyo mapana, lakini yana unene na gegedu na vidole vitano kama vikono vya nyuma. Wanapoogelea, yanatumiwa mara kwa mara kupiga kasia katika mwendo ulio chini lakini mara nyingine hutumiwa kuelekeza. Masikio yao madogo yana kunyanzi ya ngozi nje yao ili kufanya vichwa vyao vinyooke ili waogelee vyema zaidi majini. Walarasi ni mdogo kuliko tembo-bahari aliye mkubwa kabisa kati ya Pinnipedia (wanyama wenye miguu-mapezi).
Zimeundwa na dentini, pembe za walarasi ni ndefu sana na ni meno yanayoendelea kukua. Hazitumiwi kuchimbia chakula lakini huwapea usaidizi mwingi wanapojikokota barafuni au ardhini. Pia zinatumiwa kuonyesha utawala na cheo.
Ngozi ni ya hudhurungi yenye kunyanzi inayoonekana kama inabadilisha rangi kulingana na halijoto, kwa sababu wakati anapohisi joto, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi huongezeka ili kumpoza. Tendo hili humpatia walarasi sura nyekundunyekundu na huonekana kama ana madoadoa. Anapohisi baridi, utiririshi wa damu kuelekea usoni mwa ngozi hupunguzika, kumpatia sura ya kukwajuka. Tabaka ya shahamu kubwa iliyo na upana wa hadi sentimita 15 inayomkinga kutoka kwa baridi.
Sharubu zao zilizo puani ni nene na zina hali ya juu ya kuhisi na husaidia wanapotafuta chakula.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.
Walarasi (kutoka Kiing.: walrus, pia huitwa nguva aktiki au sili-pembe; Kisayansi: Odobenus rosmarus) ni mnyama mkubwa wa Bahari ya Aktiki anayefanana na nguva wa kawaida mwenye meno mawili marefu, yanayoitwa pembe pia, kama tembo.