Wadudu-kijiti au vijiti vitembeavyo ni wadudu warefu wa oda Phasmatodea (phasma = kizuka) ambao wanafanana na vijiti. Wadudu-jani au majani matembeayo wa familia Phylliidae ni wanachama wa oda hii pia.
Wadudu hawa ni wembamba na warefu isipokuwa spishi za Phylliidae ambazo ni pana. Spishi kadhaa ni wadudu warefu kabisa katika dunia. Jike la Phobaeticus chani ni mrefu kuliko wote wengine na ana urefu wa sm 36 (57 kama miguu ikinyumbulika). Muundo wa mwili ni kamafleji na unafanana na kijiti au jani. Spishi nyingi hazina mabawa au zina mabawa yameyopunguka. Mabawa ya mbele ni membamba na magumu lakini yale ya nyuyma ni mapana yakiwa yamekunjuka.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.