dcsimg

Primates ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Primates ni jina la kitaalamu la kundi la mamalia wanaojumlisha lemuri, nyani na sokwe wote pamoja na binadamu.

Kuna takriban spishi 400 za primates.

Wote wanafana na binadamu kwa namna fulani. Tofauti muhimu ni lugha.

Primates huwa na mikoni yenye vidole 5 na kucha. Wanahesabiwa kuwa na vikundi au nusuoda 2: Strepsirrhini na Haplorhini.

  • Haplorrhini (wenye pua kavu) ni pamoja na nyani, na sokwe na binadamu.
  • Strepsirrhini (wenye pua bichi) ni lemuri, komba na Aye-Aye.

Uenezaji

Primates wanaishi hasa katika maeneo ya tropiki na nusutropiki ya Afrika na Asia. Katika Amerika wako baina ya Meksiko na Arjentina ya kaskazini. Binadamu pekee alisambaa kote duniani.

Barani Afrika wako kote na idadi kubwa ya spishi wako kusini ya Sahara. Hawako Ulaya isipokuwa kundi moja huko Gibraltar (kusini mwa rasi ya Iberia) lakini inawezekana hao walipelekwa huko na binadamu. Vilevile hawako Asia ya Kaskazini na ya Kati, Australia na visiwa vya Pasifiki na maeneo karibu na ncha za dunia.

Tabia

Tabia zifuatazo zinapatikana

  • mikono inafaa kwa kushika
  • kucha ni bapa ni kucha kali za kuchimba au za kujitetea; huwa na vifinyo kwenye vidole
  • miguu ni muhimu zaidi kwa kutembea
  • uwezo wa kunusa ni mkali sana, na hafifu zaidi kwa primates wanaofanya shughuli zao mchana
  • macho ni makubwa na yote mawili yanatazama mbele, uwezo wa kuona ni wa juu
  • wanazaa watoto wachache kila safari, mimba na kipindi cha kunyonyesha wadogo inachukua muda mrefu zaidi kuliko mamalia wengine wenye ukubwa sawa
  • Ubongo ni mkubwa kulingana na mamalia wengine
  • meno ya magego si zaidi ya tatu, machonge mawili na magego madogo matatu

Ukubwa

AIna ndogo ya primates ni Lemuri-panya ya Berthe yenye urefu wa sentimita 10 pekee na uzito wa gramu 38. Aina kubwa ni ngagi (gorilla) yenye kilogramu hadi 275,

Wale wa nusuoda Strepsirrhini kwa jumla ni wadogo kuliko Haplorrhini.

Spishi kadhaa wana tofauti kubwa kati ya dume na jike; dume wa spishi hizi wanaweza kuw na uzito mara mbili kuliko jike na pia kuonyesha rangi tofauti kama nyanyi ya Papio hamadryas.

Manyoya

Mwili wa primates wengi umefunikwa kwa nywele zenye rangi baina nyeupe, kijivu, kahawia hadi nyeusi. Makofi kwa kawaida hayana nywele. Spishi kadhaa hazina nywele usoni. Binadmu ni spishi yenye nywele chache.

Viungo vya mwili

Primates wengi hukalia miti na viungo vya vinlingana na maisha yao. Kwa spishi nyingi miguu ni mikubwa na yenye nguvu zaidi kuliko mikono, isipokuwa Giboni wa Asia Kusini-Mashariki na sokwe kubwa wasio binadamu.

Spishi zinazotembea mtini kwa kuning’inia kwa mikono kidole gumba kimefifia.

Mkia ni muhimu kwa primati wengi wanaoishi mtini lakini spishi nyingine wana mkia mdogo au hawana. Nyani kadhaa wa Amerika wana mkia wa kushikilia usio na nywele upande wa chini pwenye neva muhimu.

Makazi

Inaaminiwa kuwa primates kiasili waliishi mtini na hadileo wengine wana maisha yao mtini pekee ambao hawatembei ardhini. Wengine wanaishi chini na juu pia. Wanaotembea kwenye uso wa ardhi pekee ni wachache pamoja na binadamu.

Primates wanaptikana kwenye aina mbalimbali za misitu kama vile msitu wa mvua, mikoko na pia kwenye misitu ya mlimai hadi kimo cha mita 3000 juu ya UB.

Spishi nyingine zinogopa maji lakini kuna pia aina zinazopenda maji zinajua hata kuogelea. Spishi kadhaa zimezoea mazingira ya kibinadamu zinazoishi kwenye vijiji na miji kama makaka ya Uhindini.

Kimsingi strepsirrhini (wenye pua bichi) wanafanya shughuli zao wakati wa usiku na kulala mchana lakini haplorrhini (wenye pua kavu) wanafanya shughuli zao machana na kulala usiku. Wale wanafanya shughuli zao usiku kwa jumla ni wadogo zaidi na wana uwezo mzuri zaidi wa kunusu.

Sawa na mamalia wengine wale wanaokula hasa majani wanapumzka muda mrefu zaidi wakihitaji muda mrefu kumeng'enya chakula chao.

Viungo vya Nje

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Primates: Brief Summary ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Primates ni jina la kitaalamu la kundi la mamalia wanaojumlisha lemuri, nyani na sokwe wote pamoja na binadamu.

Kuna takriban spishi 400 za primates.

Wote wanafana na binadamu kwa namna fulani. Tofauti muhimu ni lugha.

Primates huwa na mikoni yenye vidole 5 na kucha. Wanahesabiwa kuwa na vikundi au nusuoda 2: Strepsirrhini na Haplorhini.

Haplorrhini (wenye pua kavu) ni pamoja na nyani, na sokwe na binadamu. Strepsirrhini (wenye pua bichi) ni lemuri, komba na Aye-Aye.
license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri