Vingoyo ni ndege wakubwa wa jenasi mbalimbali za familia Ardeidae wenye domo refu na nyembamba lakini miguu mifupi kuliko spishi nyingine za familia hii. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Spishi moja huitwa ngojamalika. Ndege hawa wana rangi nyeupe na nyeusi, nyekundu au ya manjano. Vingoyo hula samaki hasa. Hizi ni spishi zinazojificha ndani ya uoto. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti au matete. Hata matago yamefichika kwa kawaida.