dcsimg

Msalvia (mmea) ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Msalvia (ujulikanao pia kama Salvia divinorum, sage of the diviners, ska maría pastora, seer's sage, yerba de la pastora ama kwa kifupi salvia) ni mmea ambao utumizi wa majani yake kwa njia ya kutafuna, kuvuta kama sigara au kupika kama chai unasababisha namna ya ulevi.[1] Majani ya mmea huu yana vidonge aina ya opioindi zinazosababisha ukumbusho-wazimu (hallucination).[2] Kwa vile mmea huu haujifanyiwa utafiti kwa kina, madhara yake na usalama wa matumizi yake kwa muda mrefu bado haujathibitishwa.

Majani yake hutumika pia kusafisha meno.

Asili na historia

Asili ya mmea huu ni nchi ya Mexico na humea kiasilia katika msitu wa Sierra Mazateca ya Oaxaca kwenye vivuli vilivyo na unyevu. Msalvia hufikia urefu wa kima zaidi ya mita moja na huwa na shina mraba lisilo na kitu ndani kama mimea mingine ya familia ya "mint" Lamiaceae. Leo msalvia pia hukuzwa nyumbani na hupandwa vipandikizi vya tawi au shina lake kwa vile mmea huu hutoa mbegu kwa uchache na ugumu sana.

Sheria

Mmea Msalvia umeruhusiwa katika nchi nyingi lakini matumizi yake hudhibitiwa nchini Australia, Ubelgiji, Brazil, Canada, Denmark, Estonia, Finland, Ujerumani, Italia, Japan, Korea Kusini, Poland, Hispania, Uswisi, Armenia na sehemu nyingine Marekani.[3][4] Hata Vile mmea wa msalvia umeenea sehemu tofautitofauti na miche yake huuzwa na wakulima wa miti no dawa katika nchi nyingine.

Tanbihi

  1. Salvia divinorum. Drugs.com (2018). Iliwekwa mnamo 22 June 2018.
  2. Butelman, Eduardo R; Kreek, Mary Jeanne (2015). "Salvinorin A, a kappa-opioid receptor agonist hallucinogen: Pharmacology and potential template for novel pharmacotherapeutic agents in neuropsychiatric disorders". Frontiers in Pharmacology 6. .
  3. Siebert (Legal status).
  4. Erowid (Legal status).

Marejeo

Viungo vya nje

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Msalvia (mmea): Brief Summary ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Msalvia (ujulikanao pia kama Salvia divinorum, sage of the diviners, ska maría pastora, seer's sage, yerba de la pastora ama kwa kifupi salvia) ni mmea ambao utumizi wa majani yake kwa njia ya kutafuna, kuvuta kama sigara au kupika kama chai unasababisha namna ya ulevi. Majani ya mmea huu yana vidonge aina ya opioindi zinazosababisha ukumbusho-wazimu (hallucination). Kwa vile mmea huu haujifanyiwa utafiti kwa kina, madhara yake na usalama wa matumizi yake kwa muda mrefu bado haujathibitishwa.

Majani yake hutumika pia kusafisha meno.

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri