Nyoka mabaka ni nyoka wa jenasi Chamaelycus katika familia Lamprophiidae walio na mabaka mgongoni.
Nyoka hawa ni wafupi, hadi sm 37 lakini sm 20-34 kwa kawaida. Rangi ni kijivu au kahawia na wana mabaka meusi mgongoni.
Tabia za nyoka mabaka hazijulikani sana. Inaonekana kama hukiakia ardhini usiku. Hula wadudu na mayai ya reptilia lakini mijusi pia.
Nyoka hawa hawana sumu na kwa kisa chochote wako wadogo sana na hawawezi kung'ata watu.