dcsimg

Kuchamsitu ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Kuchamsitu ni ndege wadogo wa familia Phylloscopidae. Wanafanana na shoro, kucha na kuchanyika, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi za Phylloscopus zina rangi ya kahawia au kijani mgongoni na nyeupe au njano chini. Zile za Seicercus zina rangi kali zaidi, kijani mgongoni na njano chini; zina milia kichwani na mviringo wa jicho mweupe au njano. Ndege hawa wanatokea misitu ya Afrika, Asia na Ulaya. Spishi zinazozaa katika kanda za halijoto ya wastani huhamia kusi, zile za Ulaya huenda Afrika. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 2-7.

Spishi za Afrika (na Ulaya)

Spishi za Asia

Picha

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Kuchamsitu: Brief Summary ( Swahili )