dcsimg

Bonobo ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Bonobo au Sokwe Mtu Mdogo ni jina la nyani wakubwa wa familia Hominidae wanaofanana sana na binadamu. Anatazamiwa kama spishi ya karibu zaidi na binadamu (Homo sapiens).

Spishi hii inaishi pekee katika eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa kusini kwa Mto Kongo katika eneo la Mkoa wa Équateur.

Bonobo wametazamiwa kwa muda mrefu kama aina bainifu ya Sokwe Mtu wa Kawaida (chimpanzee) akiitwa kwa majina kama chimpanzee mdogo. Lakini tangu utafiti wa mwanabilojia Mjerumani Ernst Schwarz mwaka 1928 na wenzake Waamerika Harold Coolidge na Robert Yerkes ilionekana ni spishi baidi katika jenasi Pan.

Bonobo ni spishi katika hatari ya kupotea kwa sababu inaishi katika maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pekee. Wataalamu wameona ya kwamba spishi zote za Pan hazijui kuogelea vema kwa hiyo kuna hoja ya kuwa spishi hizi mbili ziliachana baada ya kutokea kwa Mto Kongo takriban miaka milioni 1.5 – 2 iliyopita. Bonobo huishi kusini kwa Mto Kongo lakini Sokwe Mtu wa kawaida huishi pande za kaskazini kwa mto huo.

Bonobo huwa na miguu mirefu, midomo yenye rangi ya pinki na uso mweusi. Nywele juu ya kichwa zinaelea upande kuanzia katikati juu ya kichwa. Kwa jumla katika jamii zao kike mzee ana nafasi kubwa.

Wanakula hasa matunda na majani lakini wanaongeza nyama kutoka wanyama wadogo.

Viungo vya Nje

What is a Bonobo?

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Bonobo: Brief Summary ( Swahili )