dcsimg

Goregore ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Goregore, gegemela au vinuka ni ndege wa jenasi Phoeniculus katika familia Phoeniculidae. Hawa ni ndege weusi wenye mkia mrefu na domo refu jekundu au jeusi lililopindika. Mwangani kwa jua manyoya yao yana mng'ao kijani au zambarau wa metali. Kuna mabaka meupe kwa mabawa na mkia. Hupenda kuwa kwa makundi na hupiga kelele pamoja mara kwa mara wakitetea. Inaelekea kama sauti yao ni asili ya jina “gegemela”. Hula wadudu ambao wanawatafuta katika nyufa za miti kama vigong'ota. Jike huyataga mayai 2-4 ndani ya tundu la kiasilia la mti au tundu la zuwakulu au kigong'ota. Baina ya kundi la kama ndege kumi ipo jozi moja tu inayozaa. Ndege wengine wasaidia hawa wawili kutunza makinda.

Spishi

Picha

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Goregore: Brief Summary ( Swahili )